Leo June 4, 2021 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake waamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakisubiri kupandishwa kizimbani wakati wowote kuanzia sasa kusomewa mashtaka.
Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali akiwa na wenzake na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine.