Serikali imemkatia rufaa ya kupinga kuachiwa huru katika kesi ya uhujumu uchumi iliyotolewa Juni 10,2022 kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.
Sabaya amepandishwa katika Mahakama kuu kanda ya Arusha leo akitokea katika gereza kuu la Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro ambako anakabiliwa na kesi nyingine, kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho December 13, 2022.