Agosti 16, 2021 Mshtakiwa namba moja kwenye kesi ya Unyang’anyi wakutumia Silaha linalomkabili Sabaya amesema Polisi,waendesha mashtaka wamedanganywa na shataka lililopo mahakamani limetengenezwa kisiasa na kwa sababu ya chuki nakuomba Mahakama kumuachia huru.
Akiongozwa na wakili wa utetezi Moses mahuna wakati akijitetea mbele ya hakimu mfawidhi Odira Amworo huku akilengwa na machozi amesema shtaka hilo limetengenezwa kutokana na siasa zilizopo kati ya mkoa wa Arusha na Hai.
Sabaya amesema kwa wiki tatu akiwa Mkuu wa Wilaya watu walifanya jaribio la kutaka kumuua nakuwa mkimbizi kwenye nchi yake na hakuna asiyejua kwenye mamlaka ya dola ya nchi hii.Sabaya akiendelea kujitetea huku akitoa machozi amesema mashahidi wameshindwa kuthibitisha kilichotokea na kwamba vitendo vyote vilivyotajwa hajavifanya nakuomba mahakama imuachie huru.
Sabaya amesema Mashahidi wote walioletwa Mahakamani akiwemo wa 2 watano na wa nane wametengenezwa na Bakari Msangi shahidi wa sita kwa kuwa Noman alisema tarehe 10 mwezi wa 22021 akatoe Maelezo Polisi.
Sabaya amesema shahidi wa tatu wa Jamhuri Ramadhan Ayoub ambaye ni Mfanyabiashara hakuna sehemu alisema alitishiwa Silaha na hakuwahi kuleta uthibitisho wowote kutoka Polisi ukionyesha upotevu wa laini mbili zilizokuwa kwenye simu yake.
Amesisitiza Shahidi huyo aliyeletwa na Jamhuri hajawahi kuleta uthibitisho wowote Mahakamani unaoonesha alitibiwa Hospitali baada yakupigwa nakusema hakupigwa na mtu yeyote na hakuwepo kwenye duka hilo hapo.
Sabaya ameendelea kuiambia Mahakama hiyo kuwa shahidi huyo na wenzake wamesema baada ya kudai aliporwa simu nakutishiwa bastola alirudi tena kudai simu yake jambo ambalo si la kweli na shtaka lilopo Mahakamani ni la kutengeneza.
Amesema kitendo kilichofanywa na mashahidi cha kumgusa kwa lengo la kumtambua mahakamani hapo mashahidi hai wamedai hawajawahi kumuona au kukutana naye Popote isipokuwa Shahidi Bakari Msangi.
Amesema kabla ya kumtambua hapo ilipaswa ifanyike paredi ya Polisi kwa ajili ya utambuzi kwa kuwa mashahidi walioletwa mahakamani walikuwa hawamfahamu.
Lengai amesema maelezo yaliyotolewa na mashahidi na yalipo kwenye hati ya mashtaka hayaendani kwa kuwa kwenye kosa la kwanza inasemekana tukio la wizi wa fedha lilitokea tarehe February 9 2021 wakati mashahidi wanasema imetokea February 12 2021.
Kwenye hati ya mashtaka inadai tukio hilo limetokea mtaa wa Bondeni Street ila mashahidi wote wamesema tukio hilo limetokea mtaa wa sokoni kwenye duka la Shahidi store, utofauti mwingine alioutaja ni kwenye hati ya mashtaka kwamba mmiliki wa duka hilo ni Mohamed Saadi lakini shahidi namba moja aliyeapa Mahakamani ana anaitwa Mohammed Saad Hajirin.
Ameeleza kwenye mashtaka wamesema lengo kakuingia dukani hapo ilikuwa ni kupora million mbili laki sana na elfu sitini na tisa Lakini mashahididi wanasema dhamira ilikuwa ni kumtafuta mohamed Saadi Hajirin.
Kwenye hati ya mashtaka inasoma Lengai Ole Sayaba alipora fedha shilingi milioni mbili laki saba na elfu sitini lakini mashahidi wamesema hawajawahi kumuona Huku Sabaya akidai hajawahi kukutana na mtu huyo anayeitwa Sayaba.
Sabaya amesema kwenye hati ya mashtaka imeelezwa na Shahidi wa sita wa Jamhuri Bakari Msangi kuwa tukio hilo lilitokea mtaa wa Soko kuu na sio Bondeni Street kama ilivyoandikwa.
Kwenye hati ya mashtaka imeonyesha Bakari alitishiwa bunduki ili anyang’anywe fedha lakini Bakari alisema alinyooshewa bastola asachiwe ili aache kiherehere nakuacha kufuatilia mali za watu na kwamba Silaha hiyo ilitumika kumuangalia kama ana Silaha.
Amesema shahidi wa Jamhuri Said Hajirin alisema watu walikuwa wanafanyiwa upekuzi kuangaliwa kama wana Silaha.
Akiendelea kuyasoma mahstaka hayo amesema anajibu malalamiko yaliyotolewa kwa mtu anayefahamika kwa jina la Sayaba ambaye hamfahamu.
Kwenye shtaka la tatu imeandikwa Lengai Ole Sayaba aliiba shilingi elfu 35 pamoja na simu lakini shahidi wa tatu ambaye ni Ramadhan Ayubu amesema hakuona mtu yeyote aliyeiba simu yake kwa kuwa alikuwa na Wenge.
Shahidi huyo wa tatu wa Jamhuri imeelezwa kwamba hajawahi kupeleka ushahidi wowote Mahakamani ukionyesha umiliki wowote wa simu pamoja na fedha.
Akiongozwa na wakili Dankaan Sabaya amesema P3 iliyowasilishwa Mahakamani kama kielelezo kimetengenezwa makusudi kwa kuwa kinapingana na Shahidi wa 7 na wa 10 kwa kuwa P3 imeandikwa aliepigwa ni mwanamke na aliekuja mahakamani ni Mwanaume.
Amesema p3 iliandikwa na Venance Bwakisa shahidi namba 7 ambapo maelezo ya shahidi namaba 11 ambYe ni Askar alisema picha hizo zilipigwa na mtu anayefahamika kwa jina la Habibu na hazionyeshi zilipigwa tarehe ngapi.
Kielelezo namba 4 kimeonekana kimetengenezwa tarehe 24 mwezi wa 7 wakati wanamhoji Shahidi namba nne ambapo Sabaya amesema kwenye leseni ya biashara imetaja eneo la bondeni kati lakini imemtaja Mohamed saadi Hajirin biashara zake zipo Nyamwezi street nakusema ushahidi wa Mohamed hauna uhusiano kati ya maelezo pamoja na vielelezo.
Sabaya amesema kwa wiki tatu akiwa Mkuu wa Wilaya watu walifanya jaribio la kutaka kumuua nakuwa mkimbizi kwenye nchi yake na hakuna asiyejua kwenye mamlaka ya dola ya nchi hii
Katika kesi hiyo ya unyang’anyi wakutumia silaha washtakiwa ni Silvester Nyegu pamoja na Daniel Bura, Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 17,2021 ambapo mawakili wa serikali wataanza kumuuliza maswali mshatakiwa huyo.
SABAYA ATOA CHOZI, AOMBA AACHIWE HURU “WALITAKA KUNIUA, KESI IMETENGENEZWA”