Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake sita wanaoshtakiwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi wameanza kusomewa maelezo ya awali huku Jamhuri ikitarajia kuleta Mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16.
Mshtakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wanashtakiwa kwa shtaka la uhujumu Uchumi lenye makosa mbalimbali ambapo kosa la kwanza ni kuongoza genge la uhalifu pamoja na utakatishaji wa Fedha.
Akiwasomea maelezo hayo ya awali Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Mkazi Dkt Patricia Kisinda amesema Sabaya akiongozana na wenzake sita walielekea kwenye garage ya Mroso iliyopo kwa Mworombo Arusha na kumtuhumu Mfanyabiashara Francis Mroso kuingiza bidhaa kutoka Nairobi, Znz na Dubai bila kulipa kodi.
Wakili Mkuu wa Serikali Tumaini Kweka amesema wanatarajia kuwa na Mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16 kwenye kesi hiyo ambapo Hakimu ameiahirisha kesi hiyo hadi September 23 na 24 2021.