Michezo

Umeipata ya Bondia aliyefariki baada ya kupigwa Knockout? Hii hapa toka South Africa (Video)

on

Stori kutoka South Africa inahusu taarifa ya majonzi ambapo Bondia mmoja, Mzwanele Kompolo ambaye alipanda Ulingoni kwenye Pambano la ufunguzi siku ya Jumanne September 15 2015 alifariki muda mfupi baada ya kupigwa kwa knockout kwenye Round ya kwanza kabisa kwenye pambano lake na Bondia mwingine,  Siphenathi Qampi.

Marehemu Mzwanele alianguka na kupoteza fahamu akiwa kwenye Pambano hilo, baada ya jitihada za madaktari wa uwanjani hapo kuonesha hakukuwa na dalili za hali yake kuwa sawa, ilibidi apelekwe Hospitali ambapo fahamu zake hazikurudi mpaka baadaye alipofariki.

boxing_ring_1

Matukio ya Mabondia kufariki Ulingoni sio mageni Duniani, Phindile Mwelase alikuwa Bondia wa kike ambaye na yeye alifariki October 2014 South Africa baada ya damu kuvujia kwenye ubongo akiwa kwenye pambano, mwingine ni David Browne Jr ambaye alifariki Australia jumanne September 14 2015 baada ya kupigwa kwa Knockout pia kwenye pambano Australia.

Hiki hapa kipisi cha Video kifupi kilichorekodiwa dakika za mwisho za Bondia Mzwanele Kompolo uwanjani.

https://www.youtube.com/watch?v=AiesRW9cdsg

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments