Twenzetu Kigoma ndio maneno mawili ya mwanzo yanayotumika sana kwa sasa kuelekea mechi ya Simba vs Yanga itakayochezwa July 25 2021 Lake Tanganyika Stadium Kigoma,wanasema raha ya kwenda Kigoma sio ndege wala basi, raha uende na Treni….ujionee uzuri wa Tanzania na ushibe experience ya kusafiri umbali mrefu kwa treni ndani ya ardhi ya Tanzania.
Ringo Afisa wa Shirika la Reli TRC anatuelezea vitu vitakavyokuwepo kwenye treni itakayobeba mashabiki wa Simba na Yanga “Treni ipo sawasawa behewa litakalokuwa na Night Club ndio linamaliziwa, safari hii wataondoka July 23 – July 24 Saa 11 inafika Kigoma, Usalama umezingitiwa na njia zimekaguliwa, Polisi wapo”