Habari za Mastaa

Ilipoanzia Safari ya Roma na Stamina kwenye muziki mpaka kuunda ROSTAM

on

Msanii Roma ameshare safari yake na Stamina kwenye muziki ambayo ilipelekea kuundwa kwa kundi la ROSTAM ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa ya msanii Stamina, Sasa Roma ameitumia siku hii kumtakia maisha marefu Stamina kwa kutukumbusha safari yao ya kimuziki iliyounda kundi lao la ROSTAM

Roma ameeleza…. >>> Miaka Kadhaa Nyuma Lilitokea Tamasha La Fiesta Nakumbuka Lilianzia Maeneo Ya Kanda Ya Ziwa. Tamasha Lilifana Sana Lakini Wakati Linaendelea Huko Mikoani Sio Mim iWala Stamina Ambao Tulikuwa Miongoni Mwa Wasanii Wanaoshiriki Tamasha Hilo.

“Kuna Siku Stamina Akanipigia Simu (Hapo Tamasha Linaendelea Mikoani Bado) Akaniuliza Oyaaa Kaka Angu Eee Kwani Wewe Hawa Jamaa Hawajakupa Show Hata Moja!!? Nikamwambia No Brother Mimi Sijaalikwa Kushiriki Ila Niko Na Tour Yangu Ya Chaka To Chaka Na Hapa Nilipo Naitafuta Sehemu Inaitwa Katolo Geita Huko Ndani Ndani. Wanangu Akina Nay wa Mitego na Kala Jeremiah Wanapajua Vizuri Sana.

“Basi Bwana Stamina Akaniambia Aisee Yani Wale Jamaa Siku Wakinipa Jukwaa Lao Nitawaonyesha HipHop Ikoje Jukwaani!! Nikamjibu Inshallah Kaka Angu Dua Kila Ukihema….Acha Mimi Nikapungie Watu Mikono Mida Ya PA hii!! Tukacheka Wote Simu Zikakata.Ebwanaa Eee Week Kadhaa Mbele Stamina Akanipigia Kaka Ukowapi? Nina Idea Kali Sana!?? Nikamwambia Enheee Kulikoni!??

“Enheee Kulikoni!?? Akanambia Mwanangu Clouds FM Wamenipigia Simu Wananitaka Fiesta Morogoro Weekend Hii!! Sasa Idea Yangu Nataka KatiKati Ya Show Yangu Wewe Roma Utokee Kama Surprise!!! Mmmh Nikavuta Pumzi Kidogo Nikapiga Funda Moja La Glass Ya Kinywaji Flani Nilikuwa Nakunywa.

“Najua Soggydoggy Anajua Hiyo Glass ilikuwa na nini.Basi Bwana Nikamkubalia Bwana Mdogo Na Akanipa Idea Ya Show Yake Anataka Tuifanyaje!! Akaongezea kwa kunambia #Tuvae Suti Na Tukaenda Shonesha #Suti Kali Sana. Basi Billnass Atabisha…. Mxiuuu!! Siku Ya Show Ikafika Bwana Nakumbuka Mm niliondoka Dar Mida Ya Jioni Saa 12 Nikiwa Na Mama Ivan Tukawashe Kagari Ketu Tukaenda Moro Nakumbuka Stamina Alinisisitiza Nijifiche Sana Ili Iwe #Surprise Kweli Basi Hata Wasanii Wenzake Wasinione. Nikafanya Hivyo

“Ukafika Muda Wa Show Sasa Jamhuri Pale. Tulibishana Sana Na Stamina Kuwa Mimi Sasa Nipande Na Ile Kidole Cha Mwisho Juu au Nipande na VivaRoma Tukabishana Mno,Tukabishana Mno Hadi Mama Ivan Akaamua Nipande Na Viva Roma Ebwana Jukwaani Akatajwa Stamina Kupanda…Morogoro Nzima Ikasimama….Kijana Akaanza Kushambulia Jukwaa Muwa Baada Ya Muwa Akachapa Miwa Kama Minne Hivi Kisha Ndio Mimi Nipande! Ikafika Zamu Yangu Kupanda Nikasikia Lile Gari La Tongwe Its Tongwe Records Beeib.

“Weee Weee Weee Asikwambie Mtu Mdogo Wangu Lilivoanza Lile Viva Roma Tu Uwanja Mzima Hadi Wauza Kyepe Waliamka Nilipokelewa Vizuri Mnoooo!!! Haijawahi Tokea. Sasa Basi Chakusikitisha Ni Kuwa, Pale Jukwaani Niliimba Mistari Kama 12 Tuuuu!!! Nilipofika Ule Mstari Unaofata Baada Ya Watuchinje Wakatutupe Kwenye Daraja La Mkapa Mziki Ukazimwa Na Taa Kisha Nikaamrishwa Nishuke Haraka Sana. Mimi Pamoja Na Stamina.Na Show Yetu Ndio Ikaishia Hapo Na Nikafukuzwa Kukaa BackStage Na Kuamriwa Nitoke Nje Ya Uwanja.

“Wanawake Wana Mioyo Milaini Sana, #Mama Ivan Akawa Analia Sana, Huku Stamina Kanikasirikia Haongei Na Mimi. NILIJISIKIA VIBAYA SANA. Nikiwa BackStage Wasanii Wote Walinilia Buyu, Kasoro Mmoja Tu My Beautiful Sister Vanessa Mdee Yeye Aliamka Na Akaja KuniHug AKinambia You Did Great My Brother!! (Barikiwa Sana Vee Chapati) Basi Shughuli Ndio Ikaisha Hapo Tukarudi Zetu Nyumbani Dar.

“Njia Nzima Hatuongeleshani Na Wife….Tumekuja Ongeleshana Kimara Mwisho!! Tulifika Nyumbani Na Tukasahau Na Maisha Yakaendelea…… Fiesta Iliendelea Hadi Ikafika Fiesta Tanga Nyumbani Kwetu!! Na mm Nishaharibu Jukwaa La Watu, Ila Fiesta Tanga Pia Kwenda Bila Mimi Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ni Changamoto, Maana Waziri Mkuu ni Mwana FA na Waziri Wa Mambo Ya Nje Ni Matonya (One Of The Greatest Artist We Proud Of)

“Tukakaa Meza Moja Na My Boss Marehemu Ruge Mungu Amrehemu Sana. Tukaambiana Makosa Yaliyotokea Morogoro Na Tukayamaliza Na Kutangazwa Roma Nitakwepo Tanga
Cha Kusikitisha Stamina Hakualikwa Tanga. Kwahiyo Ikaonekana Kuwa Mimi Nimeenda Muharibia Stamina Morogoro Kwa, Kisha Mimi Nikapewa Tanga Yeye Hakualikwa.

“Si Ndio Stamina Akaniomba Aje Kama Surprise Naye Tanga Weeeee Nikafikiriiiiiaaaaa Nikaona Dogo Anaweza Akaja Kulipiza Huyu Kuniharibia Mkate Wangu. Nikamchomolea.Stamina Akakunja Sana Nikasema Sio Kesi.

“Basi Kwahiyo Mimi Nikaendelea Na Fiesta Huku Stamina Anahesabu Dari Msamvu Morogoro Sema Mimi Nina Roho Mbaya Eeee.? Eti Ee? Kwa Kumalizia Sasa Hadithi Yetu….Ndio Ikaja Fiesta Dar Ambayo Tukaalikwa Wote Wawili Mimi Na Stamina Kushiriki

“Usiku Mmoja Kabla Ya Show Stamina Akanambia Kaka Ile Idea Ya Moro Tuliyotaka Kuifanya Sasa Tuifanye Dar!! Nikamwambia Limeisha Hilo Tukae Tuipange. Tukaenda Maisha Club KuEnjoy Usiku Huo Huku Tukipanga Show Ya Kesho. Tukiwa Maisha Club Ndani Tukaenda WashRoom……Hamaaaad Chid Benz Huyu Hapa Zikaanza Stories…… Ndipo Likaja Wazo La Kesho Kwa Show Tupande Na Chid Aje Kama Surprise

“Na Siku Ya Show Kama Mtakumbuka Ndiyo Ile Show Ambayo Tulivaa Kama #Mabondia Na Chid Akapanda Kama Refa Wa Ndondi. Ilikuwa Show Kali Saaaanaaa.Na Usiku Wa Ile Show Ndio Usiku Ambao Liliundwa Kundi La ROSTAM Ambalo Hadi Leo Ni Miongoni Mwa Makundi Bora Kabisa Ya HipHop Africa Mashariki Na Kati.Mmoja Kati Ya Wanaounda Rostam Amezaliwa Leo. Naye Ni Stamina Tumtakie Happy Birthday Endelea Kuishi My Brother Tuna Mengi Ya Kufanya!! love You Boniventure.” –  Roma

ROSA REE KAFUNGIWA KUFANYA MUZIKI NA FAINI YA MILIONI MBILI, KILICHOMPONZA HIKI HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments