Habari za Mastaa

Sakata la Harmonize, Jeshi la Polisi limetoa tamko kwa mara ya kwanza

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu zikimuhusisha Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama Harmonize.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hadi sasa wamehojiwa Watu watano kuhusiana na sakata hilo na wapo nje kwa dhamana.
“Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32)”-MAMBOSASA
Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani”-MAMBOSASA

POLISI WAFUNGUKA KUKAMATWA KWA KAJALA, PAULA NA RAYVANY “NI SAKATA LA HARMONIZE NA PICHA ZA UTUPU”

Soma na hizi

Tupia Comments