Michezo

Salim Kikeke kuiunganisha Simba SC na QPR

on

Mtangazaji wa BBC Swahili Salim Kikeke ambaye pia ni balozi wa Simba SC jijini London Uingereza, leo kupitia ukurasa rasmi wa twitter & instagram wametangaza kuwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa club ya QPR ya England.
“Balozi wetu wa London, Salim Kikeke amekutana Mkurugenzi wa Mpira wa Miguu wa QPR, Les Ferdinand na Mkurugenzi wa Ufundi ambaye amewahi kuwa kocha wa timu hiyo, Chris Ramsey kujadili namna klabu hiyo itashirikiana nasi katika maendeleo ya soka la vijana”
.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Salim Kikeke alitangazwa kuwa balozi wa Simba SC jijini London Uingereza September 30 2019, lengo likiwa ni kukusanya mashabiki wa Simba waishio London, kuitangaza club hiyo na sasa ameanza kuitafutia connection.

Soma na hizi

Tupia Comments