Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

AyoTV

Mbwana Samatta kafikisha dakika 60 za kuichezea KRC Genk, video yake ya jana uwanjani ninayo hapa

on

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta February 20 2016 ametimiza jumla ya dakika 60 za kuitumikia klabu yake ya sasa ya KRC Genk ya Ubelgiji, alijiunga nayo mapema January 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Samatta ambaye amekuwa akiingia akitokea benchi katika mechi zake zote tatu KRC, ametimiza dakika 60 za kuitumikia Genk baada ya kupata nafasi ya kucheza kwa dakika 30 akitokea benchi katika mechi vs Lokeren, baada ya dakika ya 60 kuingia kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.

Mechi ya kwanza ya Samatta kuichezea Genk alicheza kwa dakika 17 ya pili kwa dakika 13 na jana February 20 akacheza jumla ya dakika 30 ambapo mpaka mwisho game ilikua ni 0-0 unaweza kumtazama kwenye hii video hapa chini….

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments