Michezo

Video ya Mbwana Samatta alivyowaongoza wachezaji wenzake kusherehekea ushindi wa KRC Genk wa 6-1

on

February 13 Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea kama kawaida, Ligi ambayo kwa sasa watanzania wanaifuatilia ili kumuangalia nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akicheza Ligi hiyo, klabu ya KRC Genk inayochezewa na Mbwana Samatta ilicheza leo February 13 katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Waasland Beveren.

4

KRC Genk ambayo ilikuwa imeshuka hadi nafasi ya 6, baada ya kuzidiwa point na mchezo na klabu ya Charleroi imefanikiwa kurudi nafasi yake ya tano, baada ya kuibuka na ushindi wa goli 6-1 dhidi ya klabu ya Waasland Beveren inayoshika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi ikiwa na point 26, mtanzania Mbwana Samatta aliingia dakika ya 77 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.

3

Magoli ya KRC Genk yamefungwa na Nikolaos Karelis aliyefunga magoli mawili dakika ya 10 na 31, Neeskens Kebano dakika ya 26, Leon Bailey dakika ya 27, Thomas Buffel dakika ya 72 na Christian Kabasele aliyefunga goli dakika 7 baada ya Mbwana Samatta kuingia, wakati goli la Waasland Beveren lilifungwa na Zinho Gano dakika ya 19, KRC Genk wapo nafasi ya 5 wakiwa na point 41. KRC Genk itashuka dimbani ugenini February 20 kucheza dhidi ya Lokeren.

7

5

1

2

Hii ni video ya Mbwana Samatta na wachezaji wenzake wakifurahia ushindi wa goli 6-1 wakiwa dressing room.

Great victory tonight 6-1 against #waaslandbeveren ?⚽️ #playoff1 #krcgenk #sd6 #godisgreat @samagoal

A video posted by Sebastien Dewaest (@dewaest_s06) on

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments