Michezo

Samatta ahama rasmi Aston Villa

on

Nahodha wa Taifa Stars mtanzania Mbwana Samatta hatimae amekamilisha uhamisho wake wa kudumu kuitumikia club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England.

Samatta awali alijiunga na Fenerbahce kwa mkopo akitokea Aston Villa baada ya kukaa kwa miezi sita, Villa walimtoa kwa mkopo na nafasi yake ikazibwa na Watkins.

Kimsingi mwisho wa msimu wa 2020/2021 kumaliza Samatta alipaswa kurejea Aston Villa ila ameamua kusaini mkataba wa kudumu baada ya Aston na Fenerbahce kuafikiana.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mbwana Samatta alijiunga na Aston Villa January 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji lakini akawa na wakati sio mzuri sana baada ya Corona kuingia.

Soma na hizi

Tupia Comments