Top Stories

Samatta asaini miaka mitatu Fenerbahçe

on

Mtanzania Mbwana Samatta amemalizana na klabu ya  Fenerbahçe ya Uturuki, amesaini mkataba wa miaka mitatu (2021-2024) baada ya kuichezea kwa mkopo kwa mwaka mmoja akitokea Aston Villa.

Samatta alijiunga na Aston Villa ya nchini England mwaka 2020, alicheza nusu msimu kisha akapelekwa kwa mkopo wa mwaka mmoja Fenerbahce ambao wameamua kumnunua moja kwa moja, ili kuwatumikia kwa miaka mitatu.

Mtandao wa Fenerbahce umeweka wazi kumaliza kwa Samatta ambaye atawatumikia ndani ya miaka hiyo mitatu, baada ya kuonja huduma yake kwa mwaka mmoja.

CAG ALIYOINGIA IKULU AKITEMBEA KWA MGUU, RIPOTI MKONONI

 

Soma na hizi

Tupia Comments