Michezo

Samatta kuhusu hatma yake Fenerbahce

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta anayecheza Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo akitokea Aston Villa ametoa jibu ambalo ni kama njia panda baada ya kuulizwa kuhusiana na hatma yake kama atarejea Aston Villa kutokana na mkataba wake wa mkopo kumalizika.

“Watanzania baada ya kuondoka Villa waliongea maneno makali sana kwa hiyo sijui nikirudi nitakaribishwa au nitafukuzwa, nadhani nitarudi lakini sijui kama nitakaa sababu watanzania wengi waliongea maneno makali huwezi kujua kama watakuwa wamenikasirikia”>>> Samatta

Samatta aliondoka Aston Villa mwanzo wa msimu, ikiwa amedumu na Aston Villa kwa muda wa miezi sita licha ya kuwa alisaini mkataba wa miaka minne na nusu.

Soma na hizi

Tupia Comments