AyoTV

Samatta kuikosa Watford, kocha wa Aston Villa afunguka

on

Kocha wa Aston Villa Dean Smith amethibitisha kuwa club yake ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili Mbwana Samatta akitokea club ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, Dean Smith ameweka wazi kuwa club ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mambo madogo madogo.

Smith anasema kuwa hataweza kumtumia Samatta katika mchezo dhidi ya Watford kwa sababu ya kuchelewa kwa jina lake kuwa kwenye list ya wachezaji watakaocheza kesho katika uwanja wa Villa Park dhidi ya Watford, pamoja na hayo Dean Smith amesema anahitaji mshambuliaji mwingine tena aongezwe.

Dean Smith

“Nina matumaini kwamba atakuwa mchezaji wa Aston Villa hivi karibuni, inasikitisha kuwa dili haijakamilika lakini tulimtaka na hata kama angeingia leo kwenye timu alikuwa na kipindi kimoja tu cha asubuhi cha kufanya mazoezi na timu (asingekuwa tayari kucheza vs Watford”>>>Dean Smith

Samatta muda wowote atatangazwa kama mchezaji mpya wa Aston Villa akitokea KRC Genk ya Ubelgiji alikodumu kwa miaka minne na kucheza jumla ya michezo 165 na kufunga magoli 61, Samatta mwenye umri wa miaka 27 anajiunga na Aston Villa kwa dau la pound milioni 8.5.

AUDIO: KINACHOCHELEWESHA USAJILI WA SAMATTA ASTON VILLA NDIO HIKI

Soma na hizi

Tupia Comments