Michezo

Samatta kurudi uwanjani tena

on

Nahodha wa Taifa Stars anayecheza Fenerbahce ya Uturuki Mbwana Samatta leo ametoa habari njema kuhusu maendeleo yake baada ya awali kuwa nje kwa majeruhi na kutakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki 4-6.

“Kwa wote ambao wamenitakia nipone haraka asanteni kwa meseji zenu za kunipa moyo Maendeleo ni mazuri nimeanza mazoezi mepesi ya binafsi ni imani yangu nitapona kabisa na kurudi kiwanjani”>>> Samatta

November 26 2020 Samatta aliripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 4 hadi 6 baada ya kupata shida kwenye goti lake na leo ikiwa ni wiki 3 na siku 1 toka itolewe taarifa ya jeraha lake ameanza mazoezi mepesi, Samatta amekosa jumla ya game nne za Fenerbahce kwa kuwa majeruhi.

Soma na hizi

Tupia Comments