Kiungo huyo wa Newcastle atafungiwa kwa muda mrefu baada ya kukiri kuweka dau kwenye mechi alizocheza wakati akiwa Italia.
Kwa hali ilivyo Tonali bado anaweza kucheza dhidi ya Borussia Dortmund usiku wa leo kwenye Ligi ya Mabingwa huku marufuku hiyo ikiidhinishwa.
Marufuku hiyo ya muda mrefu itamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kukosa msimu uliosalia kwa Newcastle na Euro 2024, iwapo Italia itafuzu kwa dimba hilo.
Mchezaji mwenzake wa Tonali kutoka Italia Nicolo Fagiolo tayari amepigwa marufuku ya miezi saba duniani kote kwa kukiuka sheria za kamari.
Tonali, ambaye wakala wake amedai kuwa anapambana na uraibu wa kucheza kamari, alijiunga na Newcastle kwa pauni milioni 55 msimu wa joto akitokea AC Milan.