Michezo

Yanga 1-1 Simba, Mukoko ndio Man Of The Match

on

Yanga SC November 7 2020 ilikuwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kucheza mchezo wao wa 10 wa Ligi Kuu Tanzania bara 2020/21.

Katika mchezo huo ambao Yanga walipata goli la kuongoza dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Michael Sarpong baada ya Onyango kumchezea madhambi Tusila Kisinda ndani ya 18, Joash Onyango alifuta makosa dakika ya 86 kwa kufunga goli la kichwa uliyopigwa na Luis Miquissone.

Pamoja na sare hiyo Tonombe Mukoko ambaye alikuwa ndio mchezaji bora wa mechi hiyo “Man Of The Match” alipewa zawadi ya Tsh milioni moja kutoka KCB Bank kwa uwezo wake aliounesha na kukabidhiwa cash na Mkuu wa kitengo cha Masoko KCB Bi Christina Manyenye.

Soma na hizi

Tupia Comments