Habari za Mastaa

Alikiba aweka wazi kuhusu ugonvi wake na mke wake ‘Ndoa inachangamoto’

on

Msanii Alikiba ameweka wazi kuhusu story zilizokuwa zikiendelea kati yake na mke wake zilizokuwa zikidai wawili hao kuwa wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu uliopelekea mke wake Amina kuondoka na kurudi kwao Mombasa, Alikiba ameyaongea hayo kupitia kipindi cha Ala za Roho na mtangazaji Diva.

Alikiba amesema kuwa ..>>>”“Watu wasipende kufurahia matatizo ya wenzao, au labda ni ukosefu wa kazi, hakuna jambo ambalo Mwenyezi amelihalalisha na analichukia kama talaka. Binadamu unapata wapi ujasiri wa kuchochea wenzako waachane kwenye ndoa, ni shetani tu ndio anapenda ujinga huo.”

“Shemeji yenu yupo, yupo Kazini. Ndoa ina changamoto nyingi sana, sometimes kuna migogoro mnasuluhisha, lakini sifa ya ndoa ni siri na uvumilivu. Unapopewa cheti halafu uende uka-perfom, sio masihara. Waliooa wanaelewa.”

“Wasanii wangu wa Kings Music wana nyumba yao niliwanunulia maeneo ya karibu kabisa na kwangu Tabata. Wakija kwangu ni kunisalimia au kuja kurekodi.
Vijana hawa ni kama watoto wangu, kuna muda nakaa nyumbani nawamiss na nawaita wanakuja nakaa nao, tunapiga story na kutengeneza music, lakini hawajahi kuingilia privacy yangu na Mama Keyaan. Kuna muda wanaweza wasionekane nyumbani kwa muda mrefu tu.”

 

Soma na hizi

Tupia Comments