Mix

Sasa rahisi tu kutazama BSS na LaLiga

on

Moja kati ya habari zilizotoka leo ambazo moja kwa moja zinamlenga mtanzania wa chini ni hii kutoka Star Times ambayo inamlenga mtanzania wa chini ambaye ni uhakika atapata nafasi ya kuona show ya BSS 2020 inayowagusa watoto wa kitaa.

Leo imezinduliwa promotion inayowalenga watu wa chini inayoitwa Pesa Kidogo Tu unapata burudani kibao kupitia simu yako.

Hakuna tena kuwinda remote nyumbani unaweza kuunganisha dicoder yako na application ya Stars Times kupitia simu yako na unaweza kuunganisha hadi simu tatu, hii itakuwezesha kutokwazana na watu wengine wa nyumbani sababu ya kugongana kwa vipindi.

Hii itatoa fursa kwa kwa mashabiki wa soka wa LaLiga, Europa League, UEFA National League, BSS, Copa Italia na Copa del Rey kuona burudani zote kwa urahisi zaidi.

Soma na hizi

Tupia Comments