Mawaziri Sita watatu upande wa Tanzania, na Watatu upande wa Zambia wameingia makubaliano ya kuongeza na kuimarisha ulinzi wa Bomba la Mafuta la TAZAMA kutoka Dar hadi Ndola Zambia.
Mara baada ya makubaliano hayo kufanyika, Mawaziri hao walipata nafasi ya kuzungumza na Waandishi wa habari ambapo wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya bomba hilo kubadilishiwa matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi mpaka kusafirisha mafuta safi ya Dizeli lengo likiwa ni kudhibiti kujitokeza kwa matukio ya uhalifu wa wizi wa mafuta kwenye bomba hilo.
Mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Nishati, chini ya Waziri wa Nishati January Makamba na kuhudhuriwa na Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa.
Kwa upande wa Zambia alikuwepo Waziri wa Nishati wa Zambia Mhandisi Peter Kapala, Waziri wa Ulinzi wa Zambia Mhe. Ambrose Lufuma, na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jacob Mwiimbu.