Top Stories

Mhitimu aliedukua Mtandao wa Wizara na kujilipa Mishahara kwa miezi 10 bado anasakwa

on

Imeripotiwa kwamba Polisi wa Afrika Kusini bado wanamtafuta Kijana Bright Chabota ambae ni Mhitimu wa Taaluma ya Uhandisi wa Kompyuta kwa tuhuma za kudukua database za Idara ya Afya Nchini humo na kujiajiri kama Msimamizi wa mfumo.

Chabota ambae ana asili ya Zambia alijiajiri kimagendo kama hivyo na alikuwa haendi kazini kama Wafanyakazi wengine lakini alikuwa akipokea mshahara kila mwezi toka alipodukua hiyo database June mwaka 2018.

Inaelezwa Chabota alikuwa amewaambia Wazazi wake kwamba amepata kazi nzuri na alikuwa akiwatumia kila mwezi R7000 ambayo ni zaidi ya MILIONI MOJA ya Kitanzania toka hiyo June 2018 alipodukua ambapo baadae Serikali ya Nchi hiyo iligundua kwamba amefanya kosa hilo baada ya kuonekana kuwa ni Mfanyakazi anaepokea mshahara lakini halipi kodi.

MARAFIKI WACHOKA KUOMBWA LIFT NA MWENZAO, WAMNUNULIA GARI LAKE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA WALIVYOM-SUPRISE

WEZI WALIVYOREKODIWA VIDEO BILA KUJUA WAKIIBA OFISINI DAR ES SALAAM, BOSS AONGEA… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments