Habari za Mastaa

Chris Brown am-diss mpenzi mpya wa Karrueche

on

Inaonekana kama Chris Brown hataki kuachia mapenzi aliyonayo kwa Mwanadada Karrueche baada ya wawili hao kuachana miaka mitano iliyopita, hii ni baada ya Chris Brown kuonyesha wivu kwa kumsema vibaya mpenzi wa sasa wa Karrueche, Victor Cruz.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Victor Cruz alipost picha akiwa na Karrueche , Chris Brown aliamua kudondosha comments kibao zikimuhudhi Victor na kusema kuwa hajui kuvaa na inabidi Karrueche amfundishe kupigilia mavazi kwani anaonekana kama mwanamieleka mstaafu na baadae alifuta comments hizo.

“Sio kitu kibaya au kikubwa , mboreshe basi dada au nitamzungusha ili nimpigilie pamba, sio chuki ila anahitaji kuwa na roho ya mchezo , ni amani, upendo na furaha  tafadhali mboreshe mpenzi wako” aliandika Chris Brown.

VIDEO: BEN POL KAFUNGUKA SAFARI ZAKE ZA NJE, MJENGO, MAGARI YA KIFAHARI YA KWENYE VIDEO NI YA MPENZI WAKE.?

Soma na hizi

Tupia Comments