Huku dunia ikiwa bado haijaweza kumaliza hali ya mshangao ulioibuka kufuatia taarifa za kujiuzulu kwa rais wa FIFA, Sepp Blatter.. taarifa kadhaa nyumbani kwa Rais huyo nchini Uswisi zinadai kuwa huenda akarejea tena madarakani.
Gazeti moja la kila siku nchini Uswisi la Schweiz am Sonntag limechapisha habari isemayo kuwa huenda rais huyo akarudi madarakani kufuatia kuombwa kufanya hivyo na vyama kadhaa vya soka katika mabara ya Afrika na Asia.
Headline ya Schweiz am Sonntag imeandikwa hivi >>> “Sepp Blatter soll Präsident der Fifa bleiben (Sepp Blatter to remain president of Fifa)“>>>
Chanzo kingine kilicho karibu na Blatter kimesema kuwa rais huyo amefikiria kurejea madarakani japo bado hajaweka wazi azma hiyo na kwa jinsi mambo yanavyokwenda anaweza kurudi.
Blatter alichaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa FIFA akimshinda makamu wake wa Rais, Prince Ali Bin Al Hussein kabla ya kuamua kujiuzulu siku nne baada ya uchaguzi huo kufuatia mfululizo wa kashfa za rushwa ulioikumba FIFA.
Hadi sasa viongozi kadhaa wa FIFA wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi kuhusiana na kashfa hii ambayo imesababisha mgogoro mkubwa na hali ya sintofahamu kwenye shirikisho hili la Kimataifa la mchezo wa soka.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.