Michezo

Unawajua watu ambao Rais wa FIFA Sepp Blatter anaofananishwa nao?

on

mastaaUchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA unatarajia kufanyika May 30 mjini Zurich, Uswisi huku wagombea wanne wakiwa tayari wametangaza nia ya kutaka kumrithi rais wa Shirikisho hilo, Sepp Blatter.

Blatter ameendelea kung’aa kwenye harakati za Uchaguzi huo.. huenda akashinda kwa mara nyingine baada ya wanachama kumi wa Shirikisho la soka Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Muungano wa visiwa vya Carribbean (CONCACAF) kumuunga mkono kiongozi huyo katika uchaguzi mkuu.

mastaa

Kitendo cha wanachama hao kufanya hivyo kimemfanya Blatter kufafanishwa na watu mashuhuri duniani walioweka historia na kujipatia umaarufu mkubwa kama Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela, Winston Churchill, Abraham Lincoln na Martin Luther King.

Rais wa CONCACAF, Jeffrey Webb amesema wanachama wake wanaendelea kumuunga mkono Blatter.

Wengine wanaowania Urais wa FIFA ni pamoja na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael van Praag, na Ali Bin Al Hussein.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments