Michezo

Scholes awa mbogo, Pogba mfukuze Raiola

on

Kiungo wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa ni Mchambuzi wa soka katika kituo cha BT Sport Paul Scholes ameeleza kuwa Paul Pogba anatakiwa kumzuia wakala wake Mino Raiola kutotoa maneno ya hivyo kuhusu Man United au amfukuze nafasi ya uwakilishi wake.

“Sifikiri kama club inatakiwa kujibu hilo kwa nini ampe wakala muda wa kufanya hivyo? Paul Pogba ndio tatizo kwa sababu anamlipa (Raiola) kumuwakilisha yeye (Pogba), (Raiola) anamuwakilisha vibaya na Pogba ni mtu mzuri”>>> Scholes

“Kila mmoja nje ya club atajua (Pogba) ndio ana matatizo kumbe sio, (Pogba) ana vitu viwili tu vya kufanya juu ya Raiola amwambie anyamaze au amfukuze kazi”>>> Scholes

Kauli hiyo ya Scholes inakuja ikiwa ni siku mbili zimepita toka Mino Raiola atangaze kuwa Pogba hana furaha Man United na anataka kuondoka, hii inakuja baada ya kiungo huyo wa Ufaransa kutopata nafasi ya kucheza sana kama zamani.

Soma na hizi

Tupia Comments