Leo Aprili 15, 2019 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Kongamano la Waigizaji Tanzania ambapo amewahasa mambo mbalimbali ikiwemo suala la kujitambua.
Katika kongamano hilo lililowakutanisha waigizaji mbalimbali, Dk.Mwakyembe amewataka waigizaji wa Tanzania kujua jinsi ya kujilinda kama walivyo wa Hollywood na sio kila sehemu kuonekana.
“Wenzenu wamejiwekea ukuta ndio maana thamani yao haishuki na hamna tofauti nao lakini nyinyi mara mpo sokoni mara mnaonekana kwenye miwa,” amesema huku waigizaji wakicheka.
Pia amewataka waigizaji walevi kunywea Pombe wakiwa majumbani mwao na kama wapo wazinzi basi waoe wanawake wawili badala ya kufanya hadharani.