Michezo

KRC Genk yanusurika kwa Napoli na kuvuna point yake ya kwanza, Samatta Captain

on

Club ya KRC Genk baada ya kupoteza kwa magoli sita katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya RB Salzburg ya Austria wakiwa ugenini, leo walikuwa nyumbani Luminus Arena kukipiga dhidi ya Napoli ya Italia chini ya Ulinzi wa beki wao wa zamani Koulibaly.

Koulibaly alikuwa anarudi Genk timu ambayo aliwahi kuichezea miaka ya nyuma kabla ya milango kufunguka na kwenda mbele zaidi, Genk wakiwa nyumbani Napoli walitawala mchezo kwa asilimia 63 kwa asilimia 37 ndani ya dakika 25 za kwanza Napoli wakigongesha miamba mara tatu.

Hali ambayo inaonesha kuwa KRC Genk walielemewa zaidi ila game ilifanikiwa kumalizika kwa sare tasa (0-0) na Genk kuvuna point yao ya kwanza katika michuano hiyo, sasa wana kazi ya kwenda Anfield kucheza dhidi ya Liverpool kabla ya wiki mbili tena baadae kurudiana nao, Mbwana Samatta inaonekana kwa sasa ni kama nahodha msaidizi Genk kutokana na kuvaa kitambaa cha unahodha pale anapokesekana nahodha mkuu Dewaest.

VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments