Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif pamoja na wanaounga mkono upande wake ndani ya chama hicho wametangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Mahakama Kuu Kanda ya DSM kukubali uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Lipumba kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF).
”Uamuzi huu wa Mahakama itoshe tu kusema kwamba ni mpango wa dola wenye lengo la kuihujumu na kuidhoofisha CUF hivyo nawaomba Wanachama wote wanaotuunga mkono wahamie ACT Wazalendo” Maalim Seif
“Kwetu sisi kuhama na nyadhifa zetu halina shida hilo, mimi niko tayari kuwa Mwanachama wa kawaida ndani ya ACT Wazalendo” Maalim Seif
”Kauli yangu kwa Wana-CUF na Watanzania wote, wakati ni huu, wakati ni sasa, shusha Tanga pandisha Tanga safari iendelee” – Maalim Seif
”Tumechambua vyama vyote na tukapitia Katiba zote, tukaona masharti ya ACT Wazalendo sio magumu na wametukaribisha vizuri” Maalim Seif
”Ofisi nyingi za CUF zilikuwa za watu binafsi, kwa hiyo kama wanataka kuchukua Ofisi zao wakachukue, watajuana na wenye majengo yao sio sisi tena” Maalim Seif
”Mzigo wa CUF tumeutupa, hatuna habari tena na Chama hicho, mambo hayo yamekwisha, sasa ni kusonga mbele na ACT Wazalendo” Maalim Seif
”Sio lazima niwe Kiongozi ndani ya Chama, mimi sihitaji hata nikiwa Mwanachama wa kawaida tu inatosha, ninachojali mimi ni mapambano ndani ya ACT Wazalendo na sijaweka sharti la kuwa Kiongozi” Maalim Seif
”Kuhusu Wabunge wa CUF wanaotuunga mkono, bado ni wanachama wa CUF, hilo tumewaachia wao kama wataamua kujiunga na ACT Wazalendo ni wao, kama wataamua kuendelea huko pia ni sawa, sisi hatuna maamuzi juu yao” Maalim Seif