AyoTV

VIDEO: Majibu ya Rais Magufuli kwa wanasiasa wanaotetea wahalifu

on

Rais Magufuli leo July 2, 2017 ameweka jiwe la msingi kuzindua mradi wa ujenzi, upanuzi na ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam utakaoiwezesha kuhudumia meli kubwa shughuli ambayo itachukua miezi 30 na kugharibu Tsh. 926.2b.

Aidha akihutubia katika uzinduzi huo Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali katika kulinda na kuendeleza rasilimali za Taifa huku akiwaonya baadhi ya Wanasiasa:>>>”Niwaombe pia Wanasiasa ambao wameshindwa kucontrol midomo yao na saa nyingine wanazungumza hata mambo wasiyoyajua. Unakuta Mwanasiasa anazungumza anasema hao watu wamekaa mno lock up.

“Anashindwa kuelewa hata ndugu zetu wa Marekani wale wabaya walikaa Guantanamo miaka kuliko hata mwaka mmoja. Wanaposhikwa hawa watu ambao wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi, kuna watu wamekufa zaidi ya 35, Askari zaidi ya 15 na wanaohusika ni pamoja na hao. Mtu anatoka pale anakwenda anazungumza kwamba wamekaa mno.

“Unaweza ukaona kwamba huyo lazima anahusika kwa njia moja au nyingine. Wasitufanye tukafika hapo kwa sababu wataumia. Wajifunze kufunga midomo yao wakati Serikali inafanya kazi yake.

“Kwa ujumbe huu nataka Watanzania waelewe kuwa tuna mambo makubwa katika nchi hii tunayoshughulika nayo, na ndio maana wakati mwingine unakuta ni mzaha mzaha tu, unakuta wakati mwingine mnashughulikia rasilimali za Watanzania zinazoibiwa, mtu mwingine anapinga hadharani.” – Rais Magufuli.

Soma na hizi

Tupia Comments