Michezo

Kocha wa Mbeya City kamtupia lawama muamuzi vs Simba SC

on

Kocha mkuu wa Mbeya City Ramadhan Nswanzurimo baada ya timu yake kupoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Simba SC, ikiwa timu yake iliongoza 1-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, ameonesha kukasirishwa na muamuzi wa mchezo huo ambaye alitoa faulo kwa Simba iliyowapa goli la pili dakika ya 84 lililofungwa na Meddie Kagere.

“Nimesikitishwa kwa sababu hatukustahili kupoteza huu mchezo  nafirikiri Lines 1 amefanya kitu ambacho sio cha kimpira, unaona tatizo ni kwamba refa ndio ameamua matokeo ya mchezo, kazi nzuri imefanywa na timu yangu na hongera kwa Simba, sisemi kwamba goli walilofunga halikuwa sahihi lakini muda aliotoa faulo isiyokuwa na ulazima wowote iliyozalisha goli hilo ndio tatizo langu”>>> Ramadhan Nswanzurimo

Simba SC wanaendelea kuwa nafasi ya pili kwakuwa na point 75 wakiwa wamebakiza michezo 9 wakati Yanga wanaongoza kwa point 80 wakiwa na michezo minne imesalia, Mbeya City wao wapo nafasi ya 11 wakiwa na point 40 na tayari wamecheza michezo 33 wakibakiza michezo mitano hadi kumaliza Ligi.

CHANZO: Azam TV

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments