Top Stories

Kuwajali watu wao, MultiChoise wameadhimisha wiki ya wateja

on

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeanza maadhimisho ya wiki ya wateja ambapo itaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa zawadi kwa wafanyakazi na wateja kwa muda wa mwezi mzima.

Mkuu wa huduma kwa wateja Ngwitika Mwakihesya amesema kuwa katika kipindi hicho, MultiChoice Tanzania itakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha kuwasogelea wateja karibu zaidi na kufahamu kwa kina uzoefu wao wa kupata huduma za DStv.

‘MultiChoice inaamini kuwa wafanyakazi na wateja wetu ndiyo nguzo ya ustawi wetu hivyo katika kipindi hiki tutahakikisha tunawafikia na kuwasikiliza maoni yao na hili tunalifanya ili tuweze kuboresha zaidi huduma zetu na kumfanya mteja ajisikie kuwa yeye kweli ni mfalme” alisema Ngwitika na kuongeza kuwa zoezi hilo litahusisha kuwazawadia wafanyakazi mbalimbali pamoja na wateja na pia kuwatembelea wateja wao maeneo mbalimblai ili kuwasikiliza na kupata maoni yao.

Amesisitiza kuwa kutokana na uzito huo, zoezi la kutembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na uogozi wa kampuni hiyo “Zoezi hili la kuwatembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na viongozi hivyo hata mkurugenzi mwenyewe na timu yake ya Menejimenti wataenda kuwatembelea wateja” alisisitiza Ngwitika.

 

Soma na hizi

Tupia Comments