Mix

Habari nyingine kubwa ya leo Jan 29 ni kuteuliwa kwa Ombeni Sefue

on

Kazi ya millardayo.com na AyoTV ni kukusogezea matukio yote karibu popote ulipo saa 24 ambapo tukio la sasa unalosogezewa ni kuhusu Mwanadiplomasia Ombeni Yohana Sefue kuteuliwa na kuwa Mtanzania wa kwanza kuwepo kwenye jopo la watu mashuhuri kwenye mpango wa bara la Afrika wa kujitathmini kiutawala bora. (APRM)

Katibu mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalib anayehudhuria mkutano wa umoja wa Afrika Addis Ababa amesema Katibu kiongozi huyu wa zamani Ikulu ya Tanzania ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 62, ameidhinishwa kwenye kikao cha juu cha Wakuu wa nchi za umoja wa Afrika ambao ni Wanachama wa APRM.

Jopo la watu mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri  wakuu wa nchi wanachama wa APRM kwenye uendeshaji wa huo mpango kwenye kusimamia mpango mzima wa kujitathmini ambapo Wajumbe wa jopo hilo hudumu kwa miaka minne.

Mchakato wa kuteua wajumbe hao huanzia kwenye kupendekezwa na nchi zao na baada ya mlolongo mrefu ambao una ushindani, majina ya waliokidhi vigezo hupelekwa mezani na kuidhinishwa na kikao cha juu cha APRM.

Kwenye mkutano huo Addis Ababa Mwenyekiti wa Wakuu wa nchi APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwataka washiriki vyema kuifanya APRM kuwa chombo chenye thamani Afrika kama Waasisi wake kina Benjamin Mkapa, Obasanjo na Thabo Mbeki walivyotarajia.

ULIPITWA? Tazama kwenye hii video hapa chini Makomando wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli.

Soma na hizi

Tupia Comments