Ajali

Selfie ilivyosababisha watu wawili kupoteza maisha India

on

Kama unakumbuka mwaka jana wanafunzi wawili walizama walipokuwa wanapiga selfie katika mto uliofurika katika eneo la jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh India na polisi mjini Mumbai ilitaja maeneo 15 ambayo ‘ni hatari’ kupiga Selfie baada ya msichana wa miaka 18 kuzama baharini wakati akijipiga selfie.

Utafiti wa mwaka 2016 ulionyesha kuwa vifo vingi vinavyohusisha watu kupiga Selfie vimetokea India kuliko nchi nyingine yoyote. Wasomi kutoka chuo kikuu cha Carnegie Mellon na taasisi ya mawasiliano ya Indraprastha mjini Delhi wanasema kuwa kati ya vifo 127 vinavyotokana na watu kupoiga Selfie kati ya mwaka 2014 – 2015, visa 76 vimeripotiwa India.

Wakati utafiti ukieleza hayo leo January 17 2017 imeripotiwa habari ya vijana wawili kufariki walipokuwa wanajipiga picha kwenye reli huko India. Kundi hilo la vijana lilikwenda katika station kupiga selfie mbele ya treni zilizokuwa zinawakaribia lakini walichelewa kuondoka hivyo treni ikawakanyaga.

Polisi wakizungumza Indian Express wamesema…….>>>Wakati wa kupiga picha, waliiona treni ikija wakasongea kando lakini treni nyingine ilitokezea upande wa pili na walikwama katikati, waligongwa na mojawapo ya treni hizo’

Polisi wameongeza kuwa vijana hao walimkodisha mpigaji picha mtaalamu kwa kazi hiyo……>>>’Tumeipata kamera kutoka kwa vijana iliotumika kulikuwa na picha na video, picha hizo zinathibitisha kuwa walikuwa wanaruka kutoka reli moja hadi nyengine’

AUDIO: Ukweli kuhusu mwili wa marehemu uliokutwa ndani baada ya watu kutoka kuzika, Bonyeza play hapa chini 

 

Soma na hizi

Tupia Comments