Duniani

Baba wa kichina alivyodakwa na Selfie stick kwenye bafu la wanawake Beach !!

on

Hii ishu inamtaja raia wa China, Xia Liang mwenye umri wa miaka 36 kwamba ndio haswa mtuhumiwa wa kesi ya kuingia bafu la wanawake na selfie stick, lengo lake ni ajipige selfie au?

Selfie Thing

Liang ni raia wa China ambaye aliingia Japan siku ya Ijumaa akiwa na kibali cha kuwa ndani ya nchi hiyo kwa siku sita tu za mapumziko… akaenda kutembelea kwenye fukwe moja akienjoy na watu wengine, lakini kitu kilichosababisha ajikute mikononi mwa dola ni ishu ya kukutwa akiwa chumba kimoja kilicho jirani na bafu la wanawake huku akiwa na selfie stick… kibaya zaidi ni kwamba bafu hilo kwa juu liko wazi !!

Hapa naanza kwa kunukuu ya shuhuda mmoja baada ya huyo baba kukamatwa >>> “Alikuja akiwa amevaa nguo ndefu ya kike yenye rangi ya pinki pamoja na wigi la nywele ndefu lenye rangi ya brown” >>>

Japo Polisi hawakukuta picha yoyote ya mwanamke kwenye simu ya jamaa lakini kwa ushahidi wa vitu viwili, kwanza kuingia upande wa bafu za wanawake zilizopo ufukweni akiwa na selfie stick, na pili ishu ya kuvaa nguo na wigi kama mwanamke, kuna asilimia kubwa ya ushahidi kwamba lengo la jamaa ni kuwapiga picha wanawake wakiwa bafuni !!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments