Jana jumatatu bondia maarufu duniani Manny Pacquiao aliweka wazi mikakati yake ya kuingia kwenye siasa baada ya kutangaza kuwania nafasi ya Useneta katika moja ya majimbo nchini kwake Ufilipino.
Staa huyo kwenye Mchezo wa Boxing alitangaza kuwa atagombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2016 ingawa bado hajaweka wazi atagombea kupitia chama gani.
Bondia huyo maarufu kama Pac Man alikuwa mmoja wa wawakilishi kwenye bunge la nchi hiyo baada ya kuchaguliwa na wananchi wa wilaya yake.
Pacquiao alifanikiwa kushinda mataji nane ya dunia kupitia mchezo wa ngumi lakini alishindwa katika pambano lake la mwisho dhidi ya mpinzani wake Floyd Mayweather, ikiwa ni moja ya mapambano ya kifahari kufanyika duniani katika jiji la Las Vegas, Marekani.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE