Nchini Senegal, Baraza la Katiba limechapisha orodha – ya muda – usiku wa Ijumaa Januari 12 kamkia Jumamosi Januari 13 kati ya wagombea 21 wa uchaguzi wa urais mnamo Februari 25.
Kiongozi mkuu wa upinzani, Ousmane Sonko, haonekani kwenye orodha hiyo. Orodha ya mwisho itatolewa kabla ya Januari 20.
Miongoni mwa wagombea 21 waliothibitishwa, baada ya kuchunguza nyaraka zote za faili, ni pamoja na Waziri Mkuu wa sasa, Amadou Ba ambaye ni mgombea wa kambi ya urais, pamoja na Idrissa Seck na Mahammed Boun Abdallah Dionne, wakuu wawili wa zamani wa serikali, au Aly Ngouille Ndiaye, Waziri wa zamani wa Kilimo na Mambo ya Ndani.
Kwa upande wa upinzani, meya wa zamani wa Dakar, Khalifa Sall, na Karim Wade, wa Senegalese Democratic Party (PDS) wote waliidhinishwa, ingawa ugombea wao ulikuwa umekataliwa, wakati wa uchaguzi uliopita wa 20 mwaka 19.
Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa amepewa nafasi ya kubwa ya kushinda uchaguzi huu, hayumo kwenye orodha hiyo huku akiwa amefungwa na kuhukumiwa katika kesi kadhaa za kisheria, ugombeaji wake ulionekana kuwa haukubaliki kwa kutotoa cheti cha kuthibitisha amana ya udhamini, katika hazina ya taifa kwa ajili ya uchaguzi.