Nchini Senegal, utafaji wa manusura na miili bado unaendelea Septemba 9, 2024, kufuatia janga jipya la uhamiaji haramu: mtumbwi uliokuwa na angalau abiria 150 ulipinduka siku moja kabla katika pwani ya mji wa Mbour, karibu kilomita mia moja kusini mwa Dakar.
Nchini Senegal, kwa sasa, hakuna tathmini ya uhakika: miili mitano ilipatikana mapema mchana siku ya Jumatatu, na meli ya jeshi la majini la eegal. Miili ambayo imeongezwa kwa watu wanne waliokufa maji iliyopatikana siku ya Jumapili na wavuvi waliofika kuokoa mtumbwi huo uliopinduka. Kwa jumla, watu 24 waliokolewa na wanaume watatu bado wako hospitalini.
Lakini idadi bila shaka itabadilika na kuongezeka: kwa sasa, haijulikani kwa uhakika ni abiria wangapi – 150 au zaidi? – walikuwa kwenye mtumbwi huu.
Vyovyote vile, mtumbwi huo uliondoka kwenye fukwe za Mbour siku moja kabla katikati ya alasiri, kuelekea Visiwa vya Canary, kabla ya kuzama karibu dakika thelathini baadaye, kilomita 3 kutoka pwani ya Senegal.
Wavuvi ndio walikuwa wa kwanza kuja kusaidia mtumbwi wao kuopoa miili na walionusurika na kupaza sauti.