Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza ikiwa ni siku ya pili na hizi ndio nukuu zake baada ya kuzungumza na wananchi wa Sengerema.
Sengerema Halmashauri haifanyi vizuri, haipo vizuri kwenye matumizi ya fedha, haikusanyi fedha za kutosha lakini inafuja fedha zinazoletwa, Serikali tumeamua kuleta Wakaguzi maalum kwenye Halmashauri hii kuangalia hesabu za Halmashauri”-Rais Samia
“Kuna madeni Halmashauri ya Sengereama inadaiwa, inashangaza kuona Serikali tunaongeza kila mwaka Bajeti ya dawa na vifaa tiba lakini maeneo mengine unakwenda unaambiwa dawa hakuna hii inaonesha udhaifu wa Uongozi katika eneo husika kwahiyo Sengerema tutaiangalia vizuri”-Rais Samia
“Naambiwa Wananchi Sengerema wanakosa maji kwasababu Wakala wa Maji Sengerema wanadaiwa bili za umeme, sasa kama Wananchi wanalipa kwanini washindwe kulipa na wao bili za umeme ili maji yapatikane!?, hii inaonesha kwamba Sengerema bado kuna kazi kubwa ifanye kwenye nyanja za Uongozi wa Wilaya hii na Halmashauri zake”———Rais Samia
“Sengerema kuna tatizo la Baraza la Ardhi tumetoa kibali Baraza liundwe na tutasimamia uundwaji wake ili kuondoa changamoto za ardhi Sengerema”-Rais Samia
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIVYOZINDUA MRADI WA MAJI MISUNGWI.