Michezo

Usimchukulie poa Serena Williams..!! Cheki alivyomnasa jamaa aliyemwibia iPhone yake (+Video)

on

Kama umezoea kuwaonea wanawake au wasichana basi nikupe tahadhari kwamba usiwachukulie poa hata kidogo..! Na wenyewe wanapiga zoezi kama kawaida, na ukimzingua mnaweza kumalizana poa kabisa anytime !!

Ninayo video ya sekunde 110 inayoonesha tukio zima.. Serena amekaa zake anapiga story na mtu wake, ghafla jamaa mmoja aliyekuwa pembeni yao, akachomoka na iPhone ya Serena ambayo ilikuwa mezani pembeni yake !! Sekunde chache tu baadae, Serena akashtuka kwamba simu yake haipo.

Serena Williams

Serena Williams, staa wa mchezo wa tennis duniani.

Aliinuka kimyakimya, hakuna kuitia mwizi wala nini.. kamfata jamaa na kumbana.. jamaa kweli hakubishana nae, katoa simu akamrudishia.. ule ujasiri tu wa Serena sio kitu kidogo.. cheki stori yenyewe kwenye video ilivyokuwa.

Baada ya ishu yote, Serena aliandika post kwenye ukurasa wake Instagram akasimulia ilivyokuwa mwanzo mwisho.

Screenshot_2015-11-06-02-56-10 Screenshot_2015-11-06-02-56-46

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments