Michezo

Serie A yamponza Ancelotti, Arsenal na Everton zamfuata

on

Baada ya club ya Napoli ya Italia kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake Carlo Ancelotti akiwawezesha kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya KRC Genk na kutinga hatua ya 16 bora.

Everton sasa ni kama imefunguliwa milango ya mazungumzo wakati huu ikiwa imahusishwa kumuhitaji kocha huyo, Arsenal pia inahusishwa kumuhitaji Ancelotti.

Ancelotti anafutwa kazi baada ya kuiongoza timu hiyo katika kipindi cha miezi 19, inaelezwa kuwa mwenendo wake katika Ligi ndio umepelekea uongozi wa Napoli kuchukua uamuzi wa haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi na sio Champions League.

Napoli katika Ligi Kuu ya Italia Serie A ipo nafasi ya 7 katika msimamo ikiwa na point 21 ikicheza jumla ya michezo 15 na kushinda mitano pekee, sare 6 na wamepoteza michezo minne.

Soma na hizi

Tupia Comments