Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt. Titus Kamani amesema Serikali haitawavumilia Watendaji wa Vyama vya Ushirika wasiokuwa na utaalamu katika utunzaji wa kumbukumbu na kusababisha kupatikana kwa hati zenye mashaka.
Dkt. Kamani amesema hilo katika mkutano mkuu wa pili wa chama kikuu cha Ushirika Milambo baada ya kutolewa taarifa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika ya kuwepo kwa hati zisizoridhisha katika vyama vya msingi katika chama hicho.
Akitilia mkazo katika suala la elimu msajili msaidizi wa Mkoa wa Tabora Amerta Bureta amesema alitoa muda kwa Wataalamu kwenda kwenye mafunzo lakini asilimia 95 hawakushiriki mafunzo hayo na kusema sheria itatumika kufanya maamuzi ”Mimi sitakubali kutumbuliwa kabla nyie hamjatumbuliwa”
Akijibu kwa niaba ya chama kikuu cha Milambo Hassan Magola Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Mirambo ameeleza masikitiko yake kwa kukosa umakini kwa baadhi ya wataalamu na kushindwa kuandika taarifa sasa.
Nae Mwenyekiti wa Vyama Vikuu vya Wakulima wa Tumbaku Tanzania Emmanuel Cherehani amesema kufikia March mwaka huu viongozi wa vyama vyote na wataalamu kupata elimu ya uandishiwa taarifa za hesabu.