Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali iko tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau wa michezo kuihamisha bodi ya michezo ya kubashiri kutoka Wizara ya Fedha kwenda Wizara ya Michezo ili kuinufaisha sekta ya michezo.
Kauli ya Waziri Mkuu ameitoa wakati akijibu swali la Shabani Hamisi Taletale mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambaye muuliza Waziri mkuu kuwa serikali haioni haja ya kuihamisha michezo ya kubahatisha kutoka Wizara ya Fedha kwenda wizara ya Michezo kutokana na michezo hiyo kunufaisha asilimia 5 kwenye sekta hiyo kutokana na kusimamiwa na Wizara ya Fedha.
Akijibu swali hilo Waziri mkuu amesema “bodi ya michezo ya kubahatisha iko wizara ya fedha na anayekusanya mapato ni TRA kama vile kodi zingine zinavyokusanywa na TRA na baada ya kukusanya fedha hii baraza la michezo lililoko ndani ya Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo linapata asilimia tano ya mgao wa makusanyo ya fedha kutoka katika michezo hii ya kubahatisha kwahiyo suala la uendelezaji wa michezo linabaki palepale na kuipa TRA ni kutaka kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato lakini pia kama wadau wa michezo wataona kuna haja ya kuishauri serikali sisi tunapokea ushauri na kupitia vikao vyetu tutabadilisha kanuni na sheria ili tuelekeze huko kama umuhimu upo kwaajili ya kuendeleza michezo” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa