Ni November 29, 2024 ambapo Benki ya CRDB inazindua rasmi SAMIA INFRASTRUCTURE BOND katika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City Hall jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa waliohudhuria ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff.
“Hatifungani hii ya Samia Infrastracture Bond imetokana na changamoto kubwa ambayo tunayo, kwanza ya kibajeti lakini ya mtiriko wa fedha ambayo tulikuwa na changamoto ya kutowalipa wakandarasi wetu wakimaliza kazi kwa wakati. Na baadae ndio Serikali ilituagiza kwamba tuwe wabunifu tutafute njia mbadala ya kuondokana na hizi changamoto tusikae kusubiria serikali ndio itoe suluhisho la changamoto zetu. Tunafikiria hii ndio itakuwa suluhisho la kuondoa kucheleweshwa malipo na kukamilika kazi kwa wakati na hivyo kuchelewesha huduma kwa wananchi” – Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff