Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema katika kipindi cha miezi mitano Aprili hadi Septemba 2024 tangu DP World waanze kuendesha Gati 0-7 katika Bandari ya Dar es Salaam Serikali imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 325.3.
Prof. Mkumbo amesema mapato hayo yanayotokana na shughuli za mikataba iliyoingiwa kati ya Mamlaka ya Bandari TPA na DP World ikijumuisha tozo ya pango na Tozo ya mrahaba
“Kutokana na kuongezeka kwa mapato na kupungua kwa gharama za uendeshaji kufuatia maboresho yaliyofanyika serikali kupitia TPA imeanza uwekezaji katika miradi yenye thamani ya Shilingi1.922 trilioni (USD 686.628 milioni) kwa kutumia makusanyanyo yanayopatikana. Miradi hii ni Ujenzi wa Kituo cha Kupokwa Mafuta (SRT); Ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao (Mtwara); na Ujenzi wa Gati za Majahazi (Dhow Wharf) Dar es Salaam. “ Prof. Kitila Mkumbo