Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Ndugu.Ally Hapi (MNEC) amewahimiza Wananchi wilayani Kibiti Mkoani Pwani kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora iwasaidie kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii kama ilivyo katiuka malengo ya serikali ya awamu ya sita
Akizungumza na wanachama wa CCM tawi la Kinyanya Shina namba 4,,kata ya mtawanya katika halmashauri ya wilaya ya kibiti Katibu Mkuu Hapi amesema serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya Kinyanya ambayo imegharimu shilingi milioni 50,na zahanati nsolo nayo ikipewa shilingi milioni 50,katika hospitali ya wilaya ya kibiti serikali imeshatumia zaidi ya shilingi bilion 1.6,huku ikiendelea na ukarabati wa mradi wa maji kwa milion 700 lengo ikiwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hapi amesisitiza kuhusu suala la wananchi na wanachama wa CCM kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili kupata nafasi ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu na kuwataka wakusifanye makosa kwa kushindwa kuwachagua viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi ambako ndiyo wanakopatikana viongozi bora wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo la kibiti Twaha Mpembenwe alieza namna serikali ilivyotoa fedha kwaajili ya miradi ya melaendeleo kwenye sekta ambapo serikali imetoa fedha katika awamu kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 serikali imetoa bilioni 31.6 huku awamu ya pili ya 2023 imetoa kiasi cha shilingi bilion 8.1 ambazo kwa ujumla serikali katika jimbo la kibiti imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilion 39.8 kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha akaitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika sekta ya elimu serikali imetoa zaidi ya shilingi bilion 1.4 ambazo zimetumika kujenga madarasa 71,lakini pia imetoa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya serikali ya Dk samia ambapo kiasi cha shilingi milion 528 zilitumika huku ikiongeza kiasi cha shilingi milioni 390 kwaajili ya ujenzi wa mabweni,ujenzi wa shule katika kata ya Bungu serikali imetoa milioni 528,na ujenzi wa chuo cha Veta serikali imetoa zaidi ya shilinhi milion 300 huku katika sekta ya maji serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilion 8.2