Top Stories

Serikali imetoa Bilioni 15 kununua mahindi kwa wakulima

on

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali imekwishatoa Bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

Waziri Mkuu amefahamisha hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwela, Deus Clement Sangu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Amesema siku nne zilizopita alikuwa ziarani mkoani Katavi na kujionea hali halisi ya mlundikano wa mahindi ambapo alikutana na watu wa NFRA ili aone kasi yao ya ununuzi wa mahindi hayo..

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuunganisha taasisi za NIDA na RITA kutokana na tofauti za majukumu yake. Alikuwa akijibu swali la Mhe. Abubakari Damian Asenga, mbunge wa Kilombero ambaye alishauri taasisi hizo ziunganishwe ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo alisema kwa sasa vinacheleweshwa sana.

MARAIS VYUO VIKUU WAKUTANA DSM, WATOA TAMKO “BIMA YA AFYA, MIKOPO CHANGAMOTO”

Soma na hizi

Tupia Comments