Serikali imetoa zaidi ya shilingi Billioni 2, kwa vijana wa kata ya Luchelele Jijini Mwanza kwa kuwawezesha kuwekeza katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya ziwa Victoria.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega ameeleza hayo wakati wa zoezi la uvunaji wa samaki lililofanyika katika kijiji cha kisoko kata ya Luchelele Jijini Mwanza likihusisha vijana waliopo katika Program ya Jenga kesho iliyo bora (BBT) ambapo amesema mradi wa vizimba katika eneo hilo una wanufaika 340 huku ukiwa na vizimba zaidi ya mia moja.
Katika hatua nyingie Ulega pia amesema zaidi ya tani laki nne za samaki huzalishwa hapa nchini huku mahitaji ya samaki yakiwa ni tani laki saba hivyo amewaomba wananchi kuendelea kufanya uwekezaji katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuongeza uzalishaji wa samaki hapa nchini.
Kwa upande kwa wafanyabiashara wa samaki katika eneo hilo wameiomba serikali kuweka bei elekezi ya samaki hao ili kila mfanyabiashara aweze kumudu gharama hiyo na kujingizia kipato.
#MillardAyoUPDATES