Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kuanzisha baraza la Afya ya akili nchini litakalosimamia muundo utakaoratibu sekta mbalimbali za kitaaluma na kiutendaji ili kushugulikia ufaniaisi wa suala la Afya ya akili nchini.
Majaliwa amesema hilo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua tamko la serikali kuhusu kuanzisha baraza hilo baada ya kukithiri matukio yasiyo ya kawaida yanayochangiwa na tatizo la Afya ya akili ikiwemo Wizi,mauaji na mapenzi ya jinsia moja.
“Mpango wa serikali ni kukamilisha taratibu zote za uundwaji wa baraza ili lianze kufanyakazi na kwakuwa mbunge ni kinara tutamshirikisha kwakuwa ni kinara wa Afya ya akili kuhakikisha tunaweka mpangokazi wa kutekeleza ajenda hii ya Afya ya akili” Kassim Majaliwa