Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Serikali inavyoutangaza Mlima Kilimanjaro kimataifa
Share
Notification Show More
Latest News
Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
August 15, 2022
Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania
August 15, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Serikali inavyoutangaza Mlima Kilimanjaro kimataifa
Top Stories

Serikali inavyoutangaza Mlima Kilimanjaro kimataifa

February 10, 2022
Share
2 Min Read
SHARE

*SERIKALI YAENDELEA KUUTANGAZA MLIMA KILIMANJARO KIMATAIFA*

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuutangaza mlima Kilimanjaro Kimataifa ili kukuza utalii katika mlima huo.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Maleko aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kukuza utalii wa Mlima Kilimanjaro.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikitangaza Mlima Kilimanjaro kwa kufanya Onesho la Utalii la Kimataifa la Kilifair linalofanyika mwezi Juni Mkoani Kilimanjaro kila na mbio za Kilimanjaro zinazofanyika mwezi Februari ya kila mwaka.

Ameongeza kuwa Serikali imeshiriki katika Makongamano ya Kimataifa ikiwemo World Travel Market-London, Internationale Tourismus-Börse- Ujerumani, Fitur-Hispania na Expo 2020 Dubai lengo ikiwa ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania pamoja na kuutangaza mlima Kilimanjaro.

Pia Serikali imekuwa ikishiriki katika makongamano ya Kimataifa yanayolenga kuimarisha uhifadhi na kutangaza utalii wa Mlima Kilimanjaro mfano Kongamano la Milima Mirefu Duniani (International Moutains Alliance-ITA).

Aidha, Serikali imeandaa na kushiriki katika Onesho la Kwanza la Kimataifa la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Regional Tourism Expo-EARTE) lililofanyika jijini Arusha.

Mhe. Masanja ameweka bayana kuwa Mlima Kilimanjaro ni moja ya eneo la urithi wa dunia hivyo kupitia mikutano mbalimbali ya UNESCO mlima huo hutangazwa.
Vilevile amefafanua kuwa Serikali imekuwa ikitangaza Mlima Kilimanjaro kupitia watalii wanaotembelea maeneo mbalimbali ya vivutio nchini Tanzania ambao huwa mabalozi wa kuutangaza mlima huo.

Amesema Serikali itaendelea kutumia matukio muhimu ya kitaifa kama sherehe za uhuru kuhamasisha jamii kupanda mlima Kilimanjaro.

You Might Also Like

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi

Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’

Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu

Azikwa akiwa hai huko Madaba, DC afika eneo la tukio, ‘Jambo hili ni la kinyama’

Rais Samia atoa Bilioni 15 jimboni kwa Shigongo

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA February 10, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 10, 2022
Next Article Baada ya mjadala mzito bungeni kuhusu Ngorongoro, Waziri Mkuu atoa kauli
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
Top Stories August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
Top Stories August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
Top Stories August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
Sports August 15, 2022

You Might also Like

Sports

Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania

August 15, 2022
Sports

Inter Milan wawapa Yanga cha kusema, Shaffi Dauda atia neno, Manara apigilia msumari

August 15, 2022
Sports

Barbara awatuliza mashabiki wa Simba, wataka Mzungu aachwe wana mashabiki na mbinu za Kocha

August 15, 2022
Sports

Aziz Ki Mfalme mpya town, mchezo dhidi ya Simba SC ya dhihirissha ubora wake, ‘Jemedari amwagia sifa’

August 14, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?